NAMNA YA KUPIGA HELA FOREX BILA KELELE
- amareyafrica
- May 20, 2020
- 2 min read

Forex (Foreign exchange) ni moja kati ya biashara za mtandaoni ambazo hufanyika
mara nyingi kwa siku kupita nyingine zote.
>Ni biashara inayohusisha kuuza na kununua sarafu za nchi tofauti.
Takribani dola trillion tano (5 trillion U.S. dollars) huhusika katika biashara hii kwa siku.
Kiasi hiki ni kikubwa sana ukilinganisha na soko la hisa ambalo huhusisha trillion 1.7 kwa siku.
Urahisi wa kujiingiza katika soko la FOREX, umelifanya kuwa soko lililo 'bize' kuliko mengine yote duniani.
Wawekezaji wengi wanajiingiza katika forex bila kujiuiza, je, kuna uwezekano wa juhudi hizi kuzaa matunda?
Biashara hii ina faida kadhaa, ambazo huwafanya wawekezaji kujiingiza kwake.

1: URAHISI NA WEPESI WA KUFANYA BIASHARA
Ili eweze kuanza shughuli hii unahitaji kiasi kidogo cha mtaji, hata elfu ishirini(20,000) za kitanzania inatosha kabisa.
Hakuna ukomo wa kiasi ambacho unaweza ukawekeza katika biashara hii.

2: Soko kubwa la kifedha
Wigo wa kufanya biashara kwenye FOREX ni mpana sana.
Unaweza kuchagua sarafu za kununua au kuuza kulingana na chaguo lako.
Kama ni dollar, EURO, YEN za japan, shillingi za kitanzania,yaani ni wewe tu.

3: UKWASI (LIQUIDITY)
Neno ukwasi lisikutishe sana, maana yake ni ndogo tu.
Huu ni uwezo wa kununua na kuuza sarafu muda wowote unaotaka.
Biashara hii inawatumiaji wengi, hivyo kwa kawaida kununua ama kuuza sarafu yoyote ile inawezekana muda wowote.
(japo kuna muda soko huwa linafungwa kwa muda)
4: MAKATO MADOGO YA MADALALI
Ndio....! biashara ya FOREX ina madalali. Hawa wanamkutanisha muuzaji na mnunuaji wa sarafu.
Makato yao hubadilika kulingana na sarafu zinazobadilishana.
Kwa mfano, mnunuzi akinunua dollar $1,000,000 , dalali hukata dollar $100 kama makato ya huduma yake, sawa na asilimia 0.01%.

Forex inaonesha kuwa na uwezo wa kuongeza kipato kwa wawekezaji bila hata ya kufanya kazi kubwa sana.
Ila inashangaza sana kuona wanauchumi wengi wakikataza watu kujiingiza katika biashara hii kichwakichwa.
Ubaya wa forex ni huu hapa:
1: HAKUNA UWAZI WA UHAKIKA
Soko la sarafu linaongozwa na madalali hivyo, ni ngumu sana kujua wauzaji au wanunuaji wote waliopo ili uweze kufanya uamuzi sahihi.

2:MCHAKATO WA KUAMUA BEI YA SARAFU
mchakato wa kuamua sarafu ipi inastahili kupanda au kushuka ni 'complex' sana kwa maana unashinikizwa na vitu vingi iwememo mfumuko wa bei, kushuka kwa uchumi hata utulivu wa kisiasa na nyingine nyingi
na hivyo kuifanya FOREX kuwa na tabia isiyoweza kutabirika kwa wafanyabiashara wenyewe.

3: Hatari ya kuvamiwa mtandaoni
Idadi ya madalali imeongeza kupita kasi baadhi yao wakiwa ni wezi wa mtandaoni,
hii imeharibu usalama wa mazingira ya kufanya biashara hii mtandaoni.
Baada ya yote hayo, kama bado unataka kuendelea kujihisisha na FOREX TRADE zingatia yafuatayo:
-Tumia hesabu kufanya biashara, sio hisia
-Yajue masoko vizuri
-usitegemee kutajirika mapema
-chagua madalali waliohakikiwa
baadhi ya madalali hao ni wafuatao
-IG
-LCG
Comments