HAUHITAJI PESA KUPATA PESA:
- amareyafrica
- Aug 22, 2020
- 2 min read
Updated: Aug 22, 2020
Dunia inazidi kubadilika siku hadi siku.
Fursa mpya zinazidi kujitokeza kila siku na kufanya utafutaji wa pesa kuwa rahisi.
Nitakupa njia kadhaa unazoweza kupata kipato kinono, ila ni lazima ujue kuwa ili uzifaidi ni lazima uwekeze muda kupata ujuzi maana ni kweli kuwa sio lazima uwe na degree ndo wakuajiri.

1. software developer
Software developer wanatengeneza software mbalimbali kama applications za kwenye simu au mifumo ya kwenye makampuni mbalimbali.
Hawa jamaa wanahitajika kila kona. Kwa bahati mbaya vyuo vingi haviwazalishi kwa ubora unaohitajika sokoni.
Mshahara wa wastani wa software developer kwa AFRICA ni Dollar za kimarekani millioni 30 kwa mwaka.

2. sales representative.
Sales representative ni mabalozi wa makampuni. Hawa wanasaidia kampuni husika kupata wateja wapya
au hata manunuzi mapya hivyo ni watu wa muhimu sana. Sio lazima uwe maarufu sana kuwa balozi japo itakusaidia.
Uwezo wako wa kutambua wateja wa bidhaa flani wako mahali fulani na ukaisaidia kampuni kuwapata ni BINGO.

3. IT Administrator
Ukiwa IT Administrator utaweza kufanya kazi katika 'industry' yoyote. Kazi yako itakuwa kuwa kusimamia
nyanja zote za miundombinu ya computer ya kampuni. Hii itahusisha kuweka sawa mambo ya mitandao, server za kampuni,
Ulinzi wa data za kampuni na mifumo yake.

4. Customer Service Specialist:
Ukiwa customer service specialist kazi yako ni kupokea malalamiko na maswali ya wateja.
Pia utatoa maelezo kuhusu bidhaa na huduma za kampuni husika, utachukua 'order' za wateja na kuchakata marudisho.
Mshahara wa kawaida wa hawa specialist ni dola 14 kwa lisaa limoja.

5. Digital Marketer
Biashara za mtandaoni ni kila kitu sikuizi. Hii ni kweli hasa kwa makampuni na makampuni yanajua hilo. Digital marketer anatangaza bidhaa na kutoa miongozo ya kampuni husika mtandaoni.
Makampuni lazima yawe na mtu wa kusimamia social media zao au hata kuwatangazia huduma zao.
Mshahara hutegemea na ukubwa wa watu unaoweza kuwafikia yaani followers, subscribers na wengine kama hao.

6. IT Support/Help Desk
Hawa wanafanya kazi katika team ya watu kadhaa. Kazi yao ni kutoa support katika kusimamia network ya kampuni.
Pia wanatoa msaada wa kiufundi ili mambo yaende sawa. Ku'install' hardware na software zinazohitajika ili kutimiza majukumu ya kampuni husika.
Mshahara wa wastani wa IT support ni Dollar za kimarekani 1000 kwa mwezi.

7. Data Analyst
Moja kati ya ajira ambazo unaweza ukawa unafanya nyumbani kwako na ukafanya kwa idadi ya makampuni unayodhamiria wewe mwenyewe.
Ukiwa Data Analyst, utapewa rundo la data ambazo kampuni imekusanya na watakuhitaji wewe uzichanganue. Kisha uwaambie kutokana na hizo data kampuni itatakiwa kuchukua hatua gani nyingine ile kukua na kwanini.
Uhitaji wa hawa jamaa unatarajiwa kuongezeka kwa kishindo ndani ya miaka kadhaa ijayo.
Mshahara hutegemea uzoefu na namna mikakati yako inavyosaidia kampuni.

8. Financial Analyst
Wote tunajua sekta namba moja ya kampuni ya aina yoyote ni sekta ya mapato.
Makampuni yanahitaji watu wanaoweza kuwashauri kiutaalamu katika mambo ya kifedha.
Ishu kama wakati gani ni sahii kuchukua mkopo, wakati gani wauze na kwa kiwango gani.
Hii yote inawapa hawa Financial Analyst chance kubwa sana ya kuajiriwa.
Mshahara wa wastani ni 1.7M za kitanzania kwa mwezi.

9. Graphic designer:
Hawa ndio wana'manage' image ya kampuni. Kuanzia logo management, muonekano wa matangazo na mengine.
Pia, ukiwa graphics designer unaweza ukaamua kujiajiri. Yaani wewe utakuwa unapokea 'order' za wateja wako na kuzifanya sio lazima uwe sehemu ya kampuni.

Kati ya FURSA hizi, asilimia zaidi ya 80 hazikuwepo miaka 5 iliyopita. Ni muhimu sana kwenda na kasi ya mabadiliko ya dunia ya sasa.
Komentar