ANDROID VS IOS (iPhone). IPI NI BORA ZAIDI...?
- amareyafrica
- May 24, 2020
- 2 min read
Updated: May 24, 2020

Android NA ios.
Kitaalamu tunaziita 'OPERATING SYSTEMS (OS)'.
Wakati iPhone pekee zina OS ya iOS, simu nyingine zote zina OS ya Android.
Lakini je, ipi ni bora kuliko nyingine?
Tumezilinganisha katika mitazamo 8 ifuatayo:

1: URAHISI WA KUTUMIA
iPhone zimepangiliwa kiurahisi sana, yaani ni rahisi kupata unachotafuta kiurahisi.
Lakini Android pia zimepangiliwa kiurahisi ila cha ziada ni kuwa Android inakupa mamlaka zaidi juu ya namna unavyoweza kupangilia simu yako wewe mwenyewe.

2: MUUNDO
iPhone ni simu za starehe 'luxury phones', kwa kawaida muundo wake tu utazidi simu nyingi za Android.
iPhone ni nyembamba zaidi na nyepesi zaidi.
Lakini bado kuna baadhi ya simu za Android kama SAMSUNG GALAXY na GOOGLE PIXEL zinaweza kushindana na iPhone.

3: USALAMA
Katika hili iPhone inaongoza hakuna ubishi. Hii ni kwa sababu iOS ni closed system. kwa maana ya kwamba, applications zote zinazotumika zimeidhinishwa.
Upande wa pili, Android ni open system, kwa maana ya kwamba sio lazima ziidhinishwe na kampuni husika.

4: UWEZO WA BETRI NA KUCHAJI
Kutokana na maoni ya wengi waliotumia simu aina zote, yaani za Android na iOS.
Android zikiwa katika matumizi sahihi na 'condition' nzuri zinauwezo wa kukaa na chaji mda mrefu kuliko iOS zilizo katika condition nzuri.

5: CAMERA
Uwezo wa CAMERA kwenye Android unatofautiana kulingana na aina ya simu lakini Android yenye uwezo mkubwa wa CAMERA ambayo ni GOOGLE PIXEL 4XL ikilinganishwa na
iPhone11, iPhone inazidi kuongoza.

6: UCHAGUZI WA SOFTWARE
iOS ina jumla ya apps 2.2 millioni wakati Android ina 2.8 millioni, hivyo android ina uwanja mpana zaidi.
japo ukitumia iOS huwezi ukakosa app ya kutumia.

7: PERIPHERALS (VIUNGANISHI VYA PEMBENI)
Android zote zinatumia standard USB port ambayo unaweza ukatumia kwa simu zote za android.
Lakini iPhone zinatumia LIGHTNING PORT AMBAYO ni ghali kuliko USB na utazitumia kwenye iPhone pekee.

8: VOICE ASSISTANTS
Kama unatumia iPhone, utakuwa unamjua SIRI. Huku Android kuna GOOGLE ASSISTANT. Hawa ni wasaidizi wa kidigitali.
Ni wazi kuwa GOOGLE ASSISTANT anashinda katika hii sekta.
Kwa mfano, ukiseti kwenye GOOGLE CALENDAR kuwa tarehe flani ni birthday ya rafiki yangu. GOOGLE ASSISTANT atakukumbusha kununua zawadi tarehe ikikaribia.
Mbali na hilo kuna mambo mengi sana Google Asssistant na SIRI wanaweza kukusaidia lakini GOOGLE ASSISTANT anaongoza.
Mwisho wa siku, mahitaji na uwezo wa mtu ndivyo vitakavyoweza kumfanya mtu aamue kati ya android na iOS ipi ni bora.
Kama unahitaji simu ya kipekee na nyepesi kutumia, chukua iPhone.
Kama unahitaji simu yenye uwanja mpana wa kuchagua unachotaka kuanzia muonekano mpaka software zake, chukua Android.
Comments